Ushirika wa marafiki wa Ifakara

Msaada kwa Tanzania - kampeini ya Tirol katikati ya Africa

 

Ushirika wa marafiki wa Ifakara unaona kuwa unawajibika kufadhili mradi ulioanzishwa katika mji wa Ifakara kusini mashariki mwa Tanzania mnamo mwaka 1953. Mradi huu wa maendeleo ulianzishwa na mapadre wakapuchini kutoka nchini Uswiss kwa ushirikiano na Dr. Karl Schöpf ambaye kwa sasa anaishi Zams.
Kwa kushirikiana na shirika la msaada la serikali ya Austria, serikali ya Tirol na watu wengine binafsi, ushirika wetu unaelekeza jitihada zake katika kuboresha sekta ya mafunzo na kitengo cha afya kwaajili ya wakazi, kupambana na umaskini na kuwasaidia wakazi wa Ifakara kuboresha matumizi ya rasilimali walizonazo.

PAROKIA YA MT. ANDREA

PAROKIA YA MT. ANDREA

Idara ya undugu wa kiparokia ina lengo la kuishi undugu wa kweli miongoni mwa watu wa parokia za Zams-Zammerberg-Schönwies na watu wa parokia ya Mt. Andrea, na hasa kwa majitoleo yanayofanywa na wanachama wetu katika parokia ya Ifakara. Taarifa zaidi ...

 

HOSPITALI YA MT. FRANSISKO

HOSPITALI YA MT. FRANSISKO

Idara ya hospitali ya Mt. Fransisko huifadhili hospitali teule ya Mt. Fransisko iliyoko wilayani Ifakara kwa kuipatia madawa na vifaa vya hospitali, mafunzo kwa madaktari na wauguzi, na pia kushiriki kikamilifu kwa wanachama wetu katika shughuli mbalimbali za hospitali. Taarifa zaidi ...

Foto Mainstreet

Ifakara

Ifakara mit der Pfarre St. Andrew und dem St. Francis Hospital liegt 420 km südwestlich von Dar es Salaam entfernt im Landesinneren.

Spendenkonto

Bank: Raiffeisen Bank Oberland
A-6511 Zams
Empfänger: Pfarrpartnerschaft Ifakara
IBAN Code: AT55 3699 0000 0553 2049
BIC Code: RBRTAT22